Have a sustainable water well and storage dam with value for money

FAQ

Utaratibu wa kuchimba visima ukoje?

Ukitaka kuchimba kisima unatakiwa kufanya utafiti wa awali ili:-

 • Kuangalia jiolojia ya eneo husika
 • Kuangalia uwezekano wa kuwepo mikondo ya maji ardhini
 • Historia ya eneo husika kuhusiana na suala la maji.

Gharama za kuchimba kisima zikoje?

Gharama za kuchimba kisima/Visima hutegemea zaidi mambo yafuatayo:-

 • Kipenyo na kina cha kisima pamoja na bomba zitakazotumika katika ujenzi.
 • Aina ya mwamba utakaotakiwa kutobolewa.
 • Umbali wa eneo la kuchimba kisima kutoka mahali ilipo mitambo yetu ya uchimbaji.
 • Bei ya vifaa na mafuta (Dizeli) kwa wakati husika.
 • Hali ya mazingira ya sehemu kitakapochimbwa kisima, mfano kama hakuna barabara, hivyo kuhitaji matengenezo ya njia ya kupitishia mitambo.
 • Wingi wa vifaa vitakavyotakiwa kupelekwa eneo la uchimbaji kwa ajili ya shughuli hiyo mfano booster, compresor, mudpump, generator, welding plant, mobile workshop.
 • Muda utakaotumika kupima uwezo wautoaji maji wa kisima husika.
 • Kiasi na gharama za filtergravel, polymer bentonite, diesel, lubricants nk. vitakavyotumika katika uchimbaji.
 • Gharama zote zinaweza kuandaliwa baada ya kupata ripoti ya utafiti wa eneo husika.

Gharama za ujenzi wa bwawa zikoje?

Gharama za ujenzi wa bwawa unategemea mambo yafuatayo:-

 • Uchunguzi wa mazingira.
 • Upimaji wa ardhi (Topographical Survey).
 • Utafiti wa udongo.
 • Usanifu.
 • Ripoti ya usanifu.
 • Ujenzi wa bwawa.

Kuna umuhimu gani wa kufanya utafiti kabla ya kuchimba kisima/Kujenga bwawa?

Faida za kufanya utafiti kabla ya kuchimba kisima/ kujenga bwawa ni kama ifuatavyo:-

 • Inapunguza gharamza zisizokuwa za lazima kwa eneo litakaloonekana halifai kuchimba.
 • Inapunguza hasara zitokanazo na visima visivyokuwa na maji ambavyo vilichimbwa bila kupimwa.
 • Mteja hufahamu gharama halisi kabla ya kuanza mradi.
 • Hupunguza gharama zisizokuwa za msingi kwa kuchimba kisima kirefu sababu kina cha kisima huongeza gharama.
 • Mteja hupata kisiam/bwawa bora na kilichoondaliwa kitaalamu.