Have a sustainable water well and storage dam with value for money

TUGHE

  • Event Date: Wednesday 15th, March 2017 - Friday 17th, February 2017
  • Time: 08:30 am - 03:30 am
  • Location: UDOM-DODOMA
  • Audience: Wajumbe wa baraza na menejimenti ya wakala

Baraza la wafanyakazi la Wakala limemaliza kikao cha baraza kilichofanyika viwanja UDOM mkoani Dodoma. Mgeni rasmi katika baraza hilo alikuwa Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Maji na  Umwagiliaji  Mhandisi Emmanuel Kalobero ambaye pamoja na mambo mengine aliwamwagia sifa lukuki wakala kwa kufanya kazi kwa weledi katika kutafuta vyanzo vipya vya maji kupitia uchimbaji wa visima na ujenzi wa mabwawa hasa katika ujenzi wa bwawa la Sekididi na Habia yaliyopo mikoani Simiyu na Shinyanga. Lakini pia Mhandisi kalobero amewataka wajumbe na menejimenti ya Wakala kuongeza juhudi na maarifa ili waendelee kutatua changamoto zinazowakabili na kuhakikisha wakala unasonga mbele.